HAYA NI MANENO YANGU JUU YA MSIBA HUU WA TAIFA
Kwa kweli baada ya kupokea taalifa hii ya msiba niliweza kukaa kimya kidogo niweze kutafakali
kiukweli niliona aya kwa kukaa kimya na nitakua mnafiki kama sitaungana na makamanda wengine kuwapa pole wafiwa pamoja na woote tulio au walioguswa na msiba huu
LAKINI KATIKA MSIBA HUU NIMEPATA KUJIFUNZA HAYA YAFUATAYO -:
1. Kweli kifo hakizoeleki, hata mhudumu Wa mochwari, akifiwa na nduguyake ataishia kuangua kilio wakati anapokea maiti kila siku!
2. Pamoja na falsafa kama kila apumuae ataonja mauti, kifo mipango ya mungu, binadamu bado tumeshndwa kuzoea kifo.
3. Watanzania wanaupendo wa asili, kuguswa, kuumia mmoja wameumia wote
4. Nimejifunza kifo ni kifo ila tofaut mazishi na wanaohudhuria mazishi yako
Mazishi ya first-class ni tofaut na mazishi ya lower class
5.kumbe vifo vya watoto vinagusa zaidi jamii kuliko watu wazima.
6. Kumbe kunautofauti wa hadhi ya medium school na kolomijee schools, hata kwenye majanga kama misiba namna inavyopolewa!
7. Kumbe wanasiasa hata misiba wanatumia kujinufaisha kisiasa! Msiba wanasiasa macho kodo kujitangaza
8.nimegundua watanzania wanahasira Kali kwa watoto wao, nchi nyingine ikitaka vita na Tanzania iguse mabomu kwa watoto wao,
8. Kumbe imani za kishirikina kwenye vifo Tanzania kama vile utamaduni wao, haukosi lazima wahusishe (mkono Wa mtu)
9.msiba umekuwa mkubwa sababu kila mmoja anajiona mzazi, watoto wake!
10. Police (traffic) pamoja na kutapakaa kila kona na matochi yao walishindwa, kuona hata umuhimu Wa wale wanafunzi kufunga vikanda ya usalama
Je wewe ukiwa kama rafiki yangu umejifunza nn msiba Wa Arusha???
Comments
Post a Comment