Maafisa watatu wa polisi wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulio Jumatano alfajiri eneo la Liboi Kaskazini Mashariki mwa Kenya karibu na mpaka wa Somalia.
Duru za usalama zinaarifu kuwa gari la kijeshi lililokuwa limewabeba maafisa wa usalama wa Kenya lilikanyaga bomu la kutegwa ardhini
Taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari Kenya zinasema kuwa maafisa hao walikuwa wanapiga doria katika eneo la Kulan wakati gari lao lilipokanyaga mlipuko huo.
Maafisa wengine watatu
wamejeruhiwa katika shambulio hilo na inaarifiwa wamesafirisha hadi mjini Nairobi kupokea matibabu maalumu.
Comments
Post a Comment