Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete alikuwa Brussels, Ubelgiji ambako alikutana na Mtanzania anayecheza soka la kulipwa Mbwana Samatta anayecheza katika klabu ya
K.R.C Genk.
Kupitia account yake ya twitter JK aliweka ujumbe ulioambatana na picha yake akiwa na Samatta wakati alipohudhuria Mkutano wa Wadau wa Libya na kupata nafasi ya kukutana na
Samatta.
“Nikiwa hapa Brussels kuhudhuria Mkutano wa Wadau wa Libya nimepata fursa ya kukutana na mwanasoka na kipenzi chetu” – Jakaya Kikwete.
Comments
Post a Comment