Ni dhahiri RC Makonda ni mshamba na hafikirii kwa kina

Mtu makini mara nyingi anapotaka kufanya uhuni hutumia akili nyingi sana kufanya uhuni wake,hutafakari kwa kina akishirikisha akili yake na ujanja wake afanyeje uhuni wake ufanikiwe na bado abaki salama bila kujulikana.

Mfano mzuri ni maofisini,kutokana na uwepo wa ufuatiliaji wa matumizi ya fedha,wapigaji makini hupiga kwa kutumia akili na ili ugundue ni lazima pia uwe na akili nyingi na ujanja wa kiwango chao.

Nitatoa mifano.

1.Kuwa mbwatukaji na unatumia cheti cha mtu.

2.Kumtumia "insane" kumchafua Gwajima.

Makonda hakutumia akili kabisa katika kumtumia yule dada kutaka kumchafua Gwajizzo.

Na ndio maana hata dili ikabumburuka kabla hata haijaruka hewani. Ukitazama cheti cha hospitali utaliona hili,tena alivyomshamba amekiandika kile cheti mwenyewe,halafu akaingia front mwenyewe kulazimisha "kipindi chake" kichezwe.

Huu ni ushamba.

3.Kuvamia ofisi za Clouds akiamini hatajulikana. Hivi hakuweza kufikiria hata kama kuna CCTV mle? Ni bora hata angewatuma watu wamfanyie kazi. Halafu anawatisha watu kwamba watafungwa miaka sita bila kwenda mahakamani,

huu ni ushamba wa kiwango cha lami

4.Kumuwekea loud speaker Mh.Rais

Mara kadhaa Makonda ameonekana kuongea na Rais akiwa kuweka loud speaker ili kuwaonesha watu yeye ni nani. Huu ni ushamba,"wahuni" hatuhitaji ujiko wala kutaka watu wajue sie ni kina nani. Kwa mtu wa namna ile hata kumuamini ni ngumu kwa sababu ni dhahiri hawezi kutunza siri

5.Kuweka plate namba ya RC kwenye gari binafsi

Huu ni ushamba wa madaraka. Na sio ethical kabisa,yaani ofisi yote ya RAS umekosa magari mazuri ya kutumia mpaka unaweka plate namba ya heshima kwenye gari binafsi?

Kwa hiyo uteuzi wa RC Makonda eidha haukuzingatia upekuzi au haikufanyika kwa kina. Kwa sababu kama upekuzi ungefanyika,kwa kuzingatia tu rekodi zake za chuo Makonda asingependekzwa kuwa RC Dar.

Hata record za chuo tu kwa namna alivyokuwa akifeli ni ushahidi tosha kwamba mtu huyu anauwezo mdogo wa kufikiria kwa hiyo kumpa jiji kubwa kama Dar ingekuwa kumpa mzigo.

Ni busara angepewa size yake

Comments